Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Mwanzugi akitoa tuzo kwa mwanafunzi hodari wa mwezi February anaitwa Maimuna Juma Abdala anaesoma Darasa la saba,yamefanyika haya kwa lengo la kuwamotisha wanafunzi waweze kujituma,kusoma kwa bidii na kufanya kazi mbalimbali shuleni kwa moyo.
Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Mwanzugi akitoa tuzo kwa mwalimu hodari wa mwezi February anaitwa Rashidi Idd Msuya, yamefanyika haya kwa lengo la kuwamotisha walimu waweze kujituma na kufanya kazi kwa moyo.
Tuzo hizo zinadhaminiwa na Taasisi ya Mwalimu Jipe Furaha
📢 JINSI YA KUPAKUA APP YA MWANZUGI
Ili kuendelea kupata huduma zetu kwa urahisi zaidi, fuata hatua zifuatazo kupakua App ya mwanzugi.com:
1️⃣ Fungua Google Chrome au kivinjari chochote kwenye simu yako.
2️⃣ Andika: mwanzugi.com kisha bonyeza search.
3️⃣ Ukishaingia kwenye tovuti, nenda kwenye kipengele cha “Pakua App”.
4️⃣ Bonyeza sehemu ya Download – upakuaji utaanza mara moja.
5️⃣ Baada ya kukamilika, App itaonekana kwenye uwanja wa app zote (App Menu) kwenye simu yako.
Pakua sasa na ufurahie huduma kwa haraka, salama na kwa urahisi zaidi.
Posted on March 4, 2026, 7:35 am
Uongozi wa shule unapenda kuwataarifu kuwa muda wowote kuanzia sasa, matokeo ya jaribio la mwezi Februari kwa wanafunzi wa Darasa la Tatu hadi la Saba yatatolewa rasmi kupitia mfumo wetu wa mtandaoni wa mwanzugi.com.
Tunaomba muwe tayari kufuatilia matokeo hayo kupitia akaunti zenu katika mfumo huo. Endapo kutakuwa na changamoto yoyote ya kiufundi, tafadhali wasiliana na ofisi ya shule kwa msaada zaidi.
Tunawashukuru kwa ushirikiano wenu wa karibu katika kufuatilia maendeleo ya watoto wetu. Ushirikiano wenu ni nguzo muhimu ya mafanikio yao kitaaluma.
Posted on March 3, 2026, 4:08 pm
Shule ya Msingi Mwanzugi inakutakia heri ya siku ya kuzaliwa
Posted on March 3, 2026, 2:29 pm
Wanafunzi wakigongewa nembo kwenye mashati yao
Posted on March 3, 2026, 4:55 amHii ilikuwa mwaka Jana wanafunzi wakiwa na furaha kuhitimu Elimu ya Msingi
Mwaka huu 2026 itakuwa balaa tukae tayari
Walimu wakifuahi pamoja kwa kucheza mchezo wa kujenga umakini wa kusikiliza na kutenda
Posted on March 3, 2026, 12:23 amMwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwanzugi akimsikiliza Mwanafunzi wa darasa la Awali ambae alikuwa hataki kuingia darasani na kumtatulia changamoto yake
Posted on March 3, 2026, 12:15 amMajaribio ya Kila mwezi yanaendelea na hapa ni wanafunzi wa darasa la saba wakifanya jaribio la Hisabati
Posted on March 2, 2026, 11:47 pm