🔖 Latest Blog Posts

Showing 10 of 55 posts

TUZO ZA MWEZI KWA MWANAFUNZI HODARI WA MWEZI FEBRUARY 2026

Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Mwanzugi akitoa tuzo kwa mwanafunzi hodari wa mwezi February anaitwa Maimuna Juma Abdala anaesoma Darasa la saba,yamefanyika haya kwa lengo la kuwamotisha wanafunzi waweze kujituma,kusoma kwa bidii na kufanya kazi mbalimbali shuleni kwa moyo.

Posted on March 6, 2026, 2:55 am

TUZO ZA MWEZI KWA MWALIMU HODARI WA MWEZI FEBRUARY 2026

Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Mwanzugi akitoa tuzo kwa mwalimu hodari wa mwezi February anaitwa Rashidi Idd Msuya, yamefanyika haya kwa lengo la kuwamotisha walimu waweze kujituma na kufanya kazi kwa moyo.
Tuzo hizo zinadhaminiwa na Taasisi ya Mwalimu Jipe Furaha

Posted on March 6, 2026, 2:51 am

TAARIFA KWA WAZAZI NA WALEZI

📢 JINSI YA KUPAKUA APP YA MWANZUGI
Ili kuendelea kupata huduma zetu kwa urahisi zaidi, fuata hatua zifuatazo kupakua App ya mwanzugi.com:
1️⃣ Fungua Google Chrome au kivinjari chochote kwenye simu yako.
2️⃣ Andika: mwanzugi.com kisha bonyeza search.
3️⃣ Ukishaingia kwenye tovuti, nenda kwenye kipengele cha “Pakua App”.
4️⃣ Bonyeza sehemu ya Download – upakuaji utaanza mara moja.
5️⃣ Baada ya kukamilika, App itaonekana kwenye uwanja wa app zote (App Menu) kwenye simu yako.
Pakua sasa na ufurahie huduma kwa haraka, salama na kwa urahisi zaidi.

Blog Image Posted on March 4, 2026, 7:35 am

TAARIFA KWA WAZAZI NA WALEZI

Uongozi wa shule unapenda kuwataarifu kuwa muda wowote kuanzia sasa, matokeo ya jaribio la mwezi Februari kwa wanafunzi wa Darasa la Tatu hadi la Saba yatatolewa rasmi kupitia mfumo wetu wa mtandaoni wa mwanzugi.com.
Tunaomba muwe tayari kufuatilia matokeo hayo kupitia akaunti zenu katika mfumo huo. Endapo kutakuwa na changamoto yoyote ya kiufundi, tafadhali wasiliana na ofisi ya shule kwa msaada zaidi.
Tunawashukuru kwa ushirikiano wenu wa karibu katika kufuatilia maendeleo ya watoto wetu. Ushirikiano wenu ni nguzo muhimu ya mafanikio yao kitaaluma.

Blog Image Posted on March 3, 2026, 4:08 pm

HERI YA SIKU YA KUZALIWA

Shule ya Msingi Mwanzugi inakutakia heri ya siku ya kuzaliwa

Blog Image Posted on March 3, 2026, 2:29 pm

ZOEZI LA UGONGAJI NEMBO SHULENI

Wanafunzi wakigongewa nembo kwenye mashati yao

Posted on March 3, 2026, 4:55 am

DARASA LA SABA 2025

Hii ilikuwa mwaka Jana wanafunzi wakiwa na furaha kuhitimu Elimu ya Msingi
Mwaka huu 2026 itakuwa balaa tukae tayari

Posted on March 3, 2026, 12:27 am

UPENDO DAIMA KWA KUTUMIA MICHEZO

Walimu wakifuahi pamoja kwa kucheza mchezo wa kujenga umakini wa kusikiliza na kutenda

Posted on March 3, 2026, 12:23 am

TUNAWASIKILIZA WANAFUNZI

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwanzugi akimsikiliza Mwanafunzi wa darasa la Awali ambae alikuwa hataki kuingia darasani na kumtatulia changamoto yake

Posted on March 3, 2026, 12:15 am

WANAFUNZI WAKIFANYA JARIBIO

Majaribio ya Kila mwezi yanaendelea na hapa ni wanafunzi wa darasa la saba wakifanya jaribio la Hisabati

Posted on March 2, 2026, 11:47 pm